Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mtama robo ya nne kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kimefanyika leo tarehe 30 Julai 2021 katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Yusuf Abdallah Tipu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Mh. Samwel Gunzar, Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh. Nape Moses Nnauye pamoja Katibu Tawala Wilaya Ndg. Thomas Safari na viongozi wengine.
Katika kikao hiko ziliibuka hoja na maswali mbalimbali kutoka kwa Madiwani na kutolewa ufafanuzi kutoka kwa wakuu wa idara mbalimbali.
Mganga mkuu wa wilaya ya Mtama Dkt Dismas Masulubu ametolea ufafanuzi kufuatia swali lililoulizwa na diwani viti maalumu tarafa ya Sudi mh Hawa Nameta kuhusu bima ya afya iliyoboreshwa ambapo amesema kuwa zoezi la usajili limeanza na tayari jumla ya kaya 1900 zimekamilisha usajili. Aidh Dkt Masulubu amesoma taarifa ya makusanyo ya fedha za wakulima kupitia makato ya zao la ufuta na kusema kuwa zaidi ya shilingi milioni 200 zimekusanywa, kati ya hizo shilingi mil 34 na eflu 50 zilikatwa kimakosa na tayari zimerudishwa kwa walengwa. Vilevile amesema kwamba wanajipanga ili kuhakikisha zoezi linakamilika kwa wakati na kuomba ushirikiano na madiwani kufanya kazi kwa pamoja.
Sambamba na hilo, Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh. Nape Moses Nnauye ametoa ushauri kwa Mganga Mkuu wa Wilaya pamoja na wataalamu wake kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili zoezi hilo liendelee Vizuri katika msimu wa zao la korosho.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.