Serikali ya Kijiji cha Mihima kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi imejenga ofisi bora ya Kijiji na kifunguliwa na Mhe, Shaibu Ndemanga kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Lindi tarehe 6 Januari 2021. Ofisi hiyo imejengwa kutokana na mauzo ya mazao ya maliasili ya msitu wa Kijiji hicho. Ofisi yenye thamani ya Tshs. Milioni 32.7. katika hotuba ya mgeni rasmi ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutunza misitu kwani faida ya msitu Sasa wanaiona kwani licha ya ofisi wamejenga vyumba 2 vya madarasa kwa shule ya msingi Mihima pamoja na vyoo matundu 8 na ukarabati wa barabara kwa thamani ya zaidi ya milioni 56.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.