Kampeni ya Kitaifa ya utoaji chanjo ya SURUA RUBELLA iliyoanza tarehe 15 hadi 18 Febuari 2024 imefanikiwa kwa 106.05% katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Aidha katika Halmashauri ya Mtama walengwa wa chanjo hiyo walikua 18,148 na waliopata chanjo hadi kufikia tarehe 18, Febuari 2024 ni 19,239 sawa na 106.05%.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E. Mbilinyi anaishukuru idara ya afya, wazazi, walezi na wote waliohusika katika kufanikisha malengo hayo pia utoaji wa chanjo hiyo utaendelea katika vituo vya kutolea huduma ya afya ndani ya Halmashauri.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.