Kamati ya Utawala, Fedha na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ikiongozwa na mwenyekiti wa Halmashauri Mheshimiwa Tipu Abdallah leo tarehe 15 Februari imetembelea miradi mbalimbali iliyopo Manispaa ya Lindi, miradi hiyo ni Nyumba, Ofisi na viwanja hili kufuatilia maendeleo ya miradi hiyo.
Katika mradi wa viwanja kamati imegundua kuwa Kuna wananchi waliovamia eneo hilo kwa kujenga nyumba, kilimo na shughuli nyingine, hivyo kamati itaandaa mpango mkakati wa kukutana na wananchi hao ili kufanya maamuzi sahihi.
Aidha katika mradi wa nyumba kamati imewataka wapangaji wanaodaiwa kodi kulipa kodi hizo haraka, pia imeitaka Halmashauri kuwa na mkakati wa kutunza nyumba zisizokuwa na wapangaji.
Katika mradi wa Ofisi kamati imeitaka Halmashauri kupitia upya thamani ya kodi za ofisi hizo ili Halmashauri ijiongezee kipato, lakini pia kamati imewataka wapangaji wa ofisi hizo kulipa madeni yao yote.
Mwisho kamati ilitembelea kalakana ambaopo vifaa vya Halmashauri vikiwemo magari mabovu, pikipiki na trekta vinatunzwa, hivyo basi kamati ilishauri Halmashauri iangalie namna ya kufanya mnada wa vifaa hivyo na kukodisha eneo hilo hili kuongeza mapato ya Halmashauri.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.