Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ikiongonzwa na mwenyekiti wake Mheshiwa Omari Mohamed Liveta leo tarehe 13, Febuari 2024 imetemetembelea mradi wa uchimbaji madini uliopo katika kitongoji cha Namboka, madini yanayo patikana ni madini ya vito yanayoitwa Green Garnet.
Mwenyekiti wa ulinzi wa mradi huo Mwalimu Alphonce Ngongi alieleza kuwa Halmashauri iliingia mkataba na wadhamini 16 hili kuendesha mradi huo, Mwalimu Ngongi aliongeza kuwa mgawanyo wa mauzo upo kama ifuatavyo wachimbaji watapata 50%, Halmashauri itapata 30%, Serikali ya kijiji ya Muungano II itapata 15% na wamiliki wa eneo la uchimbaji watapata 5%.
Mwalimu Ngongi aliendelea kuwa ni shimo moja pekee lililotoa madini kati ya mashimo kumi na sita, aidha Halmashauri iliweka utaratibu wa kufanya mnada wa mauzo ya madini kila jumamosi hivyo kutokana na upatikanaji wa madini kuwa mdogo wachimbaji waliomba mnada ufanyike baada ya upatikanaji wa madini kuongezeka hivyo madini yaliyo patikana yanatunzwa na Halmashauri hadi tarehe ya mnada itapopangwa.
Wachimbaji waliwasilisha changamoto zao kama ifuatavyo waliomba wafanye kazi masaa 24, waliomba Halmashauri iwasaidie vifaa vya uchimbaji hasa vifaa vya kutolea maji, waliomba Halmashauri iboreshe barabara na pia waliomba Halmashauri kuwapelekea umeme.
Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira ilifurahishwa na maendeleo ya mradi huo, Mwenyekiti wa Kamati Mheshiwa Liveta aliwataka wachimbaji kuwa wavumulivu kwasababu changamoto zao zitatatuliwa na kuwaasa wachimbaji watunze mazingira hili kujilinda na magonjwa.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.