Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi-Mtama Mhe.Othman Hongonyoko tarehe 22 Disemba 2021 ameongoza ziara ya kikazi ya Kamati ya Siasa iliyolenga kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ya Mtama ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambapo kwa asilimia kubwa Kamati hiyo iliridhishwa na maendeleo ya Miradi hiyo na kutoa pongezi kwa uongozi juu ya usimamizi imara wa kiutendaji.
Akizungumza alipofika kwenye Mradi wa Hospitali ya Wilaya iliyoko Kiwalala Mhe. Hongonyoko amesema, uwepo wa majengo mazuri ya kituo cha kutolea huduma za afya, si kitu endapo wahudumu watakuwa hawapatikiani kwa wakati, hivyo basi ametoa maelekezo kwa uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kuwasaidia watumishi wa Hospitali hiyo kupata usafiri ili iwe rahisi kwa wananchi kupata huduma ya uhakika.
Wajumbe wa Kamati wakiwa Kiwalala katika Hospitali ya Wilala
Naye Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga, amesisitiza suala la mahusiano mazuri baina ya viongozi na wananchi ili kutoa hamasa kwa wananchi hao kujitolea kwa moyo wao wote huku akiwapongeza wanajamii wa Mtama kwa kutoa ushirikiano mzuri wakati wa ujenzi wa miradi mbalimbali inayoendelea. Sambamba na hilo Mkuu wa Wilaya ameihakikishia Kamati hiyo kuwa miradi hiyo inakamilika kwa kiwango kinachoendana na thamani ya fedha.
Wajumbe wakiwa shule ya sekondari Mahiwa
Ziara hiyo, ilihusisha maeneo ya shule ya sekondari Mahiwa , Nyengedi, Mtua, kituo cha afya cha Mtama, hospitali ya Wilaya iliyoko katika Kata ya Kiwalala pamoja na kutembelea mradi wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Hospitali ya Wilaya upande wa ujenzi wa awamu ya pili
madarasa 3 shule ya sekondari Nyengedi 22/12/2021
shule ya sekondari Mtua kwa 22/12/2021
madarasa 3 Kati ya 5 shule ya sekondari Mahiwa
Wodi ya watoto Hospitali ya Wilaya
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.