Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi Ndg. Benignol Makwinya tarehe 9 Januari 2022 amewaongoza wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa kwa lengo kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa ya UVIKO 19 shule ya sekondari Mahiwa, Mtama na Mtua, ujenzi wa Ofisi za Halmashauri, Kituo cha afya Mtsma pamoja na Hospitali ya Wilaya iliyoko kata ya kiwalala ambapo Wajumbe na Mwenyekiti huyo wameridhishwa na maendeleo ya miradi hiyo.
Katika ziara hiyo Ndg. Makwinya ametoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani kwa kupeleka fedha za ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Mtama huku akitoa wito kwa wananchi pamoja na viongozi kuhakikisha mali na vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi huo vinalindwa.
Hatua ya msingi jengo la ofisi za Halmashauri Mtama
Aidha Mwenyekiti huyo alitoa rai kwa viongozi kutoa hamasa kwa wananchi wa Mtama ili waweze kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika mwaka huu 2022 ili kuisaidia Serikali kupata idadi itakayolingana na mgawanyo wa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga amesema kuwa ataendelea kusimamia kikamilifu Miradi inayoendelea huku akitoa ahadi kwa Kamati hiyo kuwa hadi kufikia mwezi wa Pili 2022 Kituo cha Afya cha Mtama kitakuwa kimekamilika.
Hatua ya skimming Kituo cha Afya Mtama
Kupitia ziara hiyo Makwinya ametoa maagizo kwa viongozi wa Halmashauri ya ya Wilaya ya Mtama kuhakikisha wanafanya ufuatiliaji wa viwanja vilivyopimwa kuwa vinamilikiwa na watu, kupanda miti eneo la hospitali ya Wilaya pamoja na kuwa na mkakati wa kuweka lami barabara inayoelekea hospitali hiyo ili kuwavutia wananchi kwenda kupata huduma za afya.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.