Kamati ya lishe Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Ndugu Anderson D Msumba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo tarehe 23 Julai 2024 imefanya kikao cha kamati kwa lengo la kutathmini taarifa ya utekelezaji wa Afua za Lishe katika Halmashauri ya Mtama kwa robo ya Nne.
Akiongea na wajumbe Mwenyekiti wa Kamati hiyo alisisitiza kuwa lishe ni suala muhimu kwani hujenga Afya iliyobora na kuondoa udumavu, hivyo basi wataalamu wa Halmashauri wanatakiwa kutoa Elimu kwa jamii hasa wazazi na walezi ili wapate uelewa zaidi kuhusu dhana ya Lishe mashuleni.
Lakini pia wakuu wa idara mbalimbali walitoa Tathmini ya Lishe katika idara husika ikiwemo idara ya Elimu na Sekondari ambapo 58% ya wanafunzi wa shule za msingi wanapata chakula shuleni huku 65 ya wanafunzi wa shule za Sekondari wanapata chakula shuleni, idara zingine ni Maendeleo ya Jamii, Kilimo,mifugo na uvuvi pamoja na idara ya Afya.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.