Kamati ya Fedha, Utawala na Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo tarehe 21 Septemba, 2021 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti Mh. Yusufu Abdallah Tipu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmshauri hiyo wakiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri Ndg. George Emmanuel Mbilinyi ilianza kukagua kituo cha mabasi Mtama ambacho pia ni chanzo cha mapato, ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa shule ya sekondari Nahukahuka yanayojengwa kwa nguvu za wananchi, zahanati ya Litipu, maabara ya sayansi shule ya sekondari Litipu, eneo la Mradi wa shamba la miwa Litipu pamoja na geti la makusanyo ya fedha zitokanazo na mgodi wa mawe Simana.
Katika ziara hiyo, Mkurugenzi Ndg. Mbilinyi alitoa pongezi kwa uongozi pamoja na wananchi wa kijiji cha Nahukahuka kwa kuwa wazalendo wa kuchangia pesha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya sekondari Nahukahuka hadi kufikia hatua ya boma. Aidha ameahidi kuhakikisha kuwa atakuwa pamoja kwa hatua iliyobakia ya ukamilishaji wa jengo hilo.
Vyumba 2 vya madarasa shule ya sekondari Nahukahuka.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.