Kamati ya afya ya msingi Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo tarehe 24 Aprili 2025 imeendesha kikao maalumu cha utoaji elimu kwa wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini kuhusu nyongeza ya dozi ya pili ya chanjo ya polio ambayo ni dozi ya sindano maarufu kama IPV2, Elimu hiyo imetolewa katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Akitoa elimu hiyo Mratibu wa chanjo Bw: Mpokwa alisema kuwa nyongeza hiyo ya chanjo itaanza kutolewa rasmi Mei 2025 na itatolewa kwa watoto wote wenye umri wa miezi 9, Bw: Mpokwa aliongeza kuwa chanjo hii ni salama kwa matumizi ya binadamu kwani imethibitishwa na shirika la Afya diniani (WHO) pamoja na mamlaka ya chakula na dawa (TMDA).
Aidha lengo la nyongeza ya chanjo hiyo ya polio ni kupunguza vifo na ulemavu unaosababishwa na ugonjwa huo, hata hivyo utoaji wa Elimu hiyo ni kuhakikisha Jamii inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu ugonjwa wa polio na chanjo zake.
Akiongea na wajumbe Mwenyekiti wa kikao hiko Mhe: Victoria Mwanziva amewataka wajumbe na wanakamati wa Afya ya Msingi kuwa mabalozi wa kuelimisha Jamii kuhusu chanjo zote hususani chanjo hiyo ya polio lakini pia hamasa itolewe Kwa wingi kuhusu umuhimu wa chanjo Kwa watoto kupitia kituo cha Redio Jamii (MTAMA FM) lakini pia chanjo iwe ajenda ya kudumu katika vikao na mikutano itakayo fanyika katika vijiji na kata .
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.