Ndiyo,Mtumishi unaposafili nje ya Kituo chako cha Kazi ni lazima uwe na kibali/ruhusa kutoka kwa Afisa Masuuli na kibali hicho kiwe kimesainiwa na Kuainishwa kwa siku ambazo utakuwa nje ya kituo chako cha kazi na kufanya hivi utakuwa umejiondolea wasiwasi ambao utaweza kukupata kama Safari yako itapata changamoto ikiwa ni pamoja na Uharibifu wa Gari njiani, ajali kwa gari ulilolipanda na kukupelekea kupata majeraha ama kupata matatizo yeyote ya ugonjwa njiani kupitia Ruhusa yako ulioiomba itaweza kukulinda haya yalisemwa na Ndg Abdallah Mnongane kutoka ofisi ya Uratibu wa utawala na Utumishi wa Umma Ikulu katika Kikao cha Watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Watumishi kutoka ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi na Ofisi ya Manispaa ya Lindi.
Mbali na hilo wawakilishi hawa kutoka Ofisi ya Uratibu wa Utawala na utumishi wa Umma Ikulu waliongelea majukumu ya Katibu Mkuu Kiongozi ambayo ni pamoja na
Pia Ndg Abdallah Mnongane kutoka Ofisi ya Uratibu wa Utawala na Utumishi wa Umma aliwasisitizia wakuu wa Idara na Vitengo kuwa wanajukumu la kuwasimamia Watumishi waliochini yao kutekeleza majukumu yao waliojiwekea baada ya Kujaza fomu ya upimaji wa Utendaji wa kazi(OPRAS) Kwani baadhi ya Watumishi wanatumia muda wa Kazi kufanya mambo yao binafsi kama vile kuendesha pipiki maarufu kama Bodaboda na pia aliwasisitizia Maafisa Utumishi kama inatokea Mtumishi wa umma amesimamishwa kazi kwa kauli ya Mwanasiasa basi Afisa utumishi atakuwa na wajibu wa Kumwandikia Barua Mtumishi huyo juu ya suala hilo na barua hiyo aeleze ni Kupumzisha kazi ili kupisha uchunguzi na siyo kumfukuza kazi maana kama hatabainika kuwa na hatia yeyote atarudishwa kazini.
Kila Taasisi ya Umma inapaswa iwe na Dawati la Malalamiko ili mtumishi mara anapoona atendewi haki aweze kufikisha malalamiko yake kwa Afisa malalamiko na pia aliongezea kuwa Afisa Malalamiko ni Mtumishi yeyote yule mwenye uzoefu wa kuijua taasisi yake, na pia kuwe na faili maalumu la Malalamiko yote yaliyoweza kuletwa na kutolewa ufafanuzi wake na yule Mtumishi aliyeleta malamiko yake aweze kupata mrejesho wa hoja zake alizowasilisha.
Kila taasisi inapaswa iweke Ratiba ya vikao vya Idara/Vitengo kwa Watumishi waliochini yao hii itasaidia kupunguza Malalamiko yaliyopo miongoni mwa Watumishi na Wananchi kwa ujumla na itasaidia kuongeza ufanisi na hali kwa Watumishi
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.