Idara ya mipango na uratibu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo tarehe 25 septemba 2024 imetembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Mtama kwa lengo la kukagua na kutathimini maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi iliyo tembelewa ni eneo la ujenzi wa shule ya sekondari ya wavulana Kiwalala, ujenzi wa zahanati ya kijiji Ruhokwe, ujenzi wa matundu 13 ya vyoo shule ya Msingi Nampunga, Ujenzi wa Zahanati ya kijij Navanga, ujenzi wa zahanati ya kijiji Mongomongo, ujenzi wa kituo cha Afya na nyumba za watumishi Pangaboi na mwisho ni eneo la ujenzi wa shule ya Sekondari Hingawali.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.