Ugonjwa huo umegundulika kwenye shamba la mahindi la Bi. Maua Mohamedi lililopo katika Kijiji cha Mvuleni Kata ya Mtama na kuathiri baadhi ya mazao hayo.
Kwa mujibu wa Afisa Kilimo na Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Bi. Violeth Byanjweli amethibitisha kupokea sampuli ya mahindi hayo na kusema kuwa ugonjwa huo haujawahi kutokea na bado hawajautambua ni ugonjwa gani hivyo basi sampuli hiyo itatumwa kwenye kituo cha utafiki wa kilimo cha Ilonga kilichopo Morogoro kwa utafiti zaidi. Ameongezea kuwa mahindi hayo hayafai kuliwa na binadamu wala mifugo.
Afisa kilimo huyo ametoa wito kwa wakulima kutumia mbegu pamoja na pembejeo bora na sahihi zinazojulikana na kuthibitishwa na wataalamu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.