Mafunzo hayo yametolewa leo tarehe 09 Julai 2021 katika shule ya msingi Mtama ambapo walioshiriki wa Mafunzo hayo ni wakuu wa shule za msingi, maafisa elimu kata, walimu wa afya pamoja na wahudumu wa afya kutoka katika zahanati na vituo mbalimbali.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo mama Sophia Chinjala ambaye ni Mratibu wa afya wilaya-mashuleni amesema kuwa lengo la serikali kuanzisha mpango huo wa kudhibiti magonjwa hayo ni pamoja na kupunguza maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine, kuua vimelea vya magonjwa hayo, kupunguza magonjwa ya ngozi , kufanya watoto wakue vizuri hivyo basi ni muhimu kuhakikisha ugawaji na matumizi ya dawa hizo ni sahihi. Aidha Mratibu huyo ametoa wito kwa wagawaji wa dawa hizo kuwa makini wakati wa zoezi hilo na kuhakikisha wanafunzi wanawapatia chakula kabla ya zoezi la ugawaji dawa halijaanza pia amewataka washiriki wote wa mafunzo hayo kuwa mabalozi wazuri kwa jamii ili kuondoa dhana potofu miongoni mwao dhidi ya dawa hizo.
Zoezi hilo linatarajiwa kuanza tarehe 12 Julai 2021 huku walengwa wakiwa ni wanafunzi wa shule za msingi walioandikishwa na wasiosndikishwa kuanzia umri wa miaka mitano hadi 14. Jumla ya shule za msingi 79 katika halmashauri ya Wilaya ya Mtama zitaendesha zoezi hilo.
Zoezi la ugawaji dawa hufanyika kila mwaka chini ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Magonjwa Yasiyopewa Kipaumbele (NTD).
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.