Bodi ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Leo tarehe 5/07/2024 imefanya kikao cha Utekelezaji wa shughuli za idara kwa mwaka 2023-2024, Kikao hiko kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Akiongea na wajumbe Ndugu Mohamedi H. Chilumba Mwenyekiti wa kikao hiko alisema kuwa wataalamu wa idara hiyo wanapaswa kuhakikisha wanaendelea kufanya hamasa kwa wananchi juu ya ujengaji na matumizi sahihi ya choo bora ili kuepukana na magonjwa ya milipuko.
Aidha Mlezi wa Mkoa wa Lindi Dr. Enock Chilumba alimpongeza Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuitendea haki idara ya Afya kwa kutoa fedha moja kwa moja zinazo saidia kununua vifaa tiba pamoja na ujenzi wa wa vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali lakini pia aliipongeza Halmashauri ya Mtama kwa kufanya vizuri katika utoaji wa chanjo na kutekeleza agizo la Serikali kwa kununua viua dudu 800.
Mwisho,Mwenyekiti pamoja na wajumbe walipiga picha za pamoja kwa ajili ya kumbukumbu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.