Idara ya Afya Halmashauri ya Wilaya ya Mtama imefanya kikao kazi kwa kiwashirikisha Watumishi wote wa Afya, Waganga wafawidhi wa vituo vya Afya na zahanati.Kikao hicho kimefanyika Tarehe 5 Januari 2021 katika ukumbi wa mikutano Mtama. Akielezea lengo la kikao hicho Ndg Dismas Masurubu Mganga mkuu wa Wilaya ni kujengeeana uwezo kiutendaji katika kusimamia ukusanyaji wa mapato kupitia mifuko ya NHIF na ICHF kwa kutumia mfumo wa FAAS. Aidha alitoa msisitizo kwa watumishi wote wa idara ya Afya kufanya kazi kwa weledi na kikao hicho kiweze kuleta tija kiutendaji na kuboresha mapato. Washiriki nao kwa upande wao walieleza changamoto wanazokutana nazo katika utendaji na kuahidi kuyatekeleza yote yaliyoagizwa kupitia kikao hicho, Mweka hazina, Mkaguzi wa ndani pamoja na watumishi wa IT ni miongoni mwa washiriki na kutoa michango yao ya kiutaalamu
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.