Mafunzo hayo yametolewa kwa Wakuu wa idara na vitengo vyote vya Halmashauri. Mwezeshaji wa mafunzo ni Ndg Nestory Mgimwa kutoka OR TAMISEMI. Lengo la mafunzo hayo ni kupunguza urasimu wa kuanzisha madai na madeni kwa watumishi kwa njia ya mfumo ujulikanao - MADENIMIS . Mfumo huu utarahisisha namna ya kuwasilisha madai na madeni , lakini pia ufuatiliaji wa hatua mbalimbali na upo wazi kwa wahusika. Baada ya mafunzo hayo ya siku mbili kuanzia Tarehe 20/8- 21/8/2020. Timu ya kushughulikia madeni ya Wilaya itaundwa na kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wote.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.