Shirika lisilo la Kiserikali la HEART TO HEART FOUNDATION Novemba 25, 2021 limehitimisha utekelezaji wa Mradi wa WASH (Water Sanitation and Hygiene) uliotekelezwa ndani ya miaka 3 kuanzia 2019-2021 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na kutoa msaada wa vitu mbalimbali vilivyokuwa vinatumika kwenye usimamizi wa Mradi huo ikiwa ni pamoja na Gari aiana ya Toyota Prado, Kompyuta mpakato 3, Printa, cabinet ndogo na projecta.
Vifaa hivyo vilitolewa kwenye hafla ya kuhitimisha Mradi huo, ambapo ulifanyika mkutano wa wadau mbalimbali kutoka ngazi ya Mkoa, Halmashauri ya Mtama na Manispaa ya Lindi pamoja na wadau wa Maendeleo Heart to Heart Foundation na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Korea Kusini (KOICA) katika Ukumbi wa Sea View Beach Resort uliopo Lindi Mjini ambapo taarifa mbalimbali za utekelezaji zilitolewa.
Aidha Vitendea kazi hivyo vimetolewa kwa ajili ya matumizi ya Idara kuendelea kufanya ufuatiliaji na usimamizi wa shughuli mbalimbali za afya, maji na usafi wa mazingira ili kuzuia maambukizi ya magonjwa ya kuhara kwa watoto chini ya miaka 5 na watu wazima.
Hand-over Ceremony
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emanuel Mbilinyi alitoa shukurani kwa uongozi wa awamu ya sita kwa kuendelea kuruhusu mashirika mbalimbali kuendelea kutoa misaada huku akiwaomba wadau wa shirika hilo kitofunga milango ya ushirikiano katika Halmashauri ya Mtama pindi tu utakapohitajika msaada katika ufuatiliaji pamoja na uendelezaji wa miundombinu waliyoiacha. Aidha, Ndg. Mbilinyi alitumia fursa hiyo kutoa shukirani za pekee kwa shirika hilo kupitia kampuni ya KOIKA kwa kutoa gari itakayosaidia kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ndani ya Halmashauri hiyo.
DED akitoa neno la shukurani.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Dismas Masulubu, aliahidi kuwa vifaa hivyo vitatunzwa kwa umakini wa hali ya juu .
DED na DMO Mtama DC wakisaini makabidhiano
Heart to Heart Foundation Tanzania kupitia WASH ililenga kuchangia katika kupunguza magonjwa ya kawaida yanayohusiana na Maji na Usafi wa Mazingira kwa kuboresha upatikanaji wa maji, usafi wa mazingira na usafi. Hivyo basi umefanikiwa kutekeleza Miradi ya maji na ujenzi wa vyoo katika Kata ya Navanga, Nachunyu, Mnolela, Kiwalala, Longa, Mtua, Nyengedi, Majengo, Mtama, Namupa, Mandwanga, Chiponda na Nyangao. Wakati huo huo kwa upande mwingine shule zote zimefikiwa kwa kupata vifaa vya kunawia mikono, utoaji wa elimu ya mabadiliko ya tabia kwa walimu na wanafunzi hasa kuacha kujisaidia haja kwenye maeneo ya wazi na uchafunzi wa vyanzo vya maji. Vituo vya kutolea huduma za afya waliwezeshwa kupata vifaa mbalimbali vya usafi wa vituo n.k.
Baadhi ya watumishi wa Mtama DC wakiwa kwenye mkutano huo
Washiriki wa mkutano wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla hiyo
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.