Mkurugenzi Msaidizi wa Uratibu na Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bi Esther Riwa akimkabidhi Hundi ya kiasi cha shilingi milioni sita na laki tano(6,500,000/=) Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Ndg Gervas Ngomano makabidhiano haya yamefanyika kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji. na katikati ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Eng Mbaraka Kilangai akishuhudia makabidhiano hayo
Mkurugenzi Msaidizi wa uratibu na uwezeshaji wa Vijana kiuchumi kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Ajira na wenye ulemavu ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi kutoa Fedha hizo(Revolving Fund) kwenye vikundi Vya vijana vyenye sifa na zenye uhitaji wa fedha hizo na akasisitiza kuwa Fedha hizi siyo Ruzuku zinapaswa zirudishwe ili ziweze kusaidia vikundi vingine vya Ujasiliamali.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Eng Mbaraka Kilangai Aliwahakikishia kuwa Fedha Hizi zitatumika Ipasavyo kama ilivyokusudiwa mana lengo kubwa ni kuondokana na umasikini uliokithiri kwa vijana wetu, na Halmashaur ya Wilaya ya Lindi imeendelea kutenga asilimia kumi ya Mapato yetu ya ndani kwa Vijana na Wakinamama
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.