Zoezi la usambazaji wa chanjo ya corona limefanyika leo katika vituo maalumu vilivyotengwa kwa ajili ya kutoa chanjo hiyo chini ya usimamizi wa mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Mtama bw. Musa Mmanga.
Akitoa elimu kwa watumishi wa afya hospitali ya Nyangao, Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Mtama bw. Mmanga ametoa wito kwa watumishi wa afya hospitali hiyo kujitokeza kwa wingi ili wapatiwe chanjo hiyo. Aidha amewahasa watumishi hao kupuuzia uzushi unaoendelea katika mitandao ya kijamii kuhusiana na chanjo hiyo na badala yake wawe na imani kwani chanjo hizo ni salama na zimethibishwa na TFDA, maabara kuu ya serikali pamoja na mkemia mkuu wa serikali.
Mratibu wa chanjo Mtama DC (wa kwanza kulia) akitoa maelekezo ya utoaji wa chanjo hizo.
Dozi 750 zimesambazwa katika vituo mbalimbali ikiwemo Hosptali ya Nyangao, Kituo cha afya cha Mtua, zahanati ya Mnolela pamoja na kituo cha afya cha Pangatena. Huduma ya chanjo hizo imelenga zaidi kutolewa kwa makundi ya watumishi walio katika hali hatarishi ambao ni watumishi wa afya, walimu pamoja na askari. Aidha watu wasiostahili kupatiwa chanjo hizo ni watu wenye umri chini ya miaka 18, watu wenye dalili na waliowahi au wenye ugongwa wa Covid19.
Tayari zoezi la utoaji chanjo limeanza katika vituo mbalimbali vilivyotengwa kwa ajili ya huduma hiyo na julma ya Watumishi 750 wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.
Mtumishi wa afya hospitali ya Nyangao akipatiwa chanjo
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.