Wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo tarehe 19 Aprili 2024 wamefanya vikao na Wavuvi, Wakulima wa Mwani, Beach Management Unit(BMU) pamoja na wenyeviti wa vijiji kutoka kijiji cha Sudi, Mmumbu, Shuka na Mongomongo, Vikao hivyo vililenga kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwenye vijiji hivyo kama vile changamoto na maoni kutoka kwa wavuvi na wakulima.
Aidha vikao viliaza kwa kutambua idadi ya vikundi vya uvuvi na Wakulima wa mwani ambavyo vimesajiliwa na Halmashauri, kwa ujumla kuna vikundi 8 vya uvuvi na vikundi 21 vya wakulima wa mwani.
Lakini pia wavuvi walielezea changamoto zao kama vile kukosa mwalo (soko la kuuza samaki), vifaa venye uwezo mdogo, kukosekana kwa wachuuzi aidha wakulima wa mwani walisema kuwa wanakumbwa na changamoto ya kushuka kwa bei, kukosa vifaa Kama vile kamba na boti pamoja na uhaba wa wanunuzi.
Alikadhalika Bi Vaileth Richard Afisa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri alisema amezipokea changamoto hizo na zitafanyiwa kazi pia aliongeza kuwa Halmashauri ipo mbioni kutoa mikopo ya boti kwa vikundi vilivyokidhi vigezo kama ambavyo ilitoa mikopo hiyo hapo mwanzo, Mwisho CPA Siliwe Mweka hazina wa Halmashauri alisema kuwa ili kutatua changamoto ya soko la samaki kuna mradi wa ujenzi wa Mwalo hivyo kijiji chenye takwimu nzuri ya ukusanyaji wa mapato kitapewa kipaumbele kwenye mradi huo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.