Ni kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mh. George Emmanuel Mbilinyi alipokutana na Madiwani, Watendaji wa kata pamoja na Watendaji wa vijiji kutoka katika kata za Madangwa, Mnolela, Pangatena, Sudi, Nachunyu pamoja na Navanga kwenye kikao kazi ili kujadili njia bora ya udhibiti wa utoroshwaji wa mazao lengo likiwa ni kuhakikisha Halmashauri hiyo inainuka kimapato. Kikao hicho kimefanyika Septemba 12 2021 katika viwanja vya Shule ya sekondari ya Madangwa .
Ikiwa kipaumbele cha kwanza ni kuinua mapato ya Halmashauri, Mh. George Mbilinyi akiwa na timu yake ya kikosi kazi ametoa maelekezo kwa wajumbe wa kikao hicho na kusema kuwa "kila kata iunde kamati za ukusanyaji wa mapato zitakazojumuisha Maafisa Tarafa, Madiwani, Watendaji wa kata pamoja na Watendaji wa vijiji na kwamba Madiwani watakuwa wasimamizi wakuu wa kamati hizo, kila kijiji kiweke vizuizi kwenye maeneo muhimu , aidha kikosi kazi kitafuatilia mwenendo wa utekelezaji wa maagizo na endapo kutakuwa na ubabaishaji katika ukusanyaji wa mapato viongozi wa eneo husika watawajibika , vilevile kila kijiji kitawekewa malengo ya makusanyo kwa kila mwezi na kwamba kila wiki kutakuwa na mrejesho wa namna ulivyokusanya, sambamba na hilo, kila Mtendaji wa kata atapimwa kulingana na mapato kwa kila chanzo kwa kulinganisha na malengo aliyopewa, ni vizuri kutengeneza mfumo wa ushirikishwaji kwa ngazi zote za uongozi, watendaji wa kata wanatakiwa kufanya vikao na kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa maagizo na kutoa ripoti kwa Mkurugenzi kila baada ya siku mbili, hivyo basi ili tufikie malengo yetu ya kuinua mapato, wakusanyaji wanatakiwa kuweka benki fedha walizokusanya kwa wakati pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato lengo ni kuifanya Halmashauri kuwa bora na kuleta maendeleo kwa wananchi". Alisema George Mbilinyi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
"MTAMA KWANZA KWA MAENDELEO"
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.