Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Mbilinyi amekutana na wakuu wa shule za msingi na sekondari pamoja na Maafisa Elimu Kata kwenye kikao kazi (Mkutano wa Maabara ya Elimu) kilicholenga kupeana mikakati ya kuinua sekta ya Elimu hususani suala la ufaulu wa wanafunzi katika Halmashauri hiyo.
Kupitia kikao hicho Mkurugenzi aliwapongeza Maafisa Elimu wa Wilaya kwa kuandaa mkutano huo huku akitoa msisitizo kwa walimu pamoja na Maafisa Elimu Kata kuandaa vikao kwenye maeneo yao ya kazi na kuwasilisha maagizo na mikakati iliyotolewa kwenye mkutano huo.
Aidha amewataka viongozi hao kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wanatakiwa kujitoa katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na usimamizi wa miradi mbalimbali na utoaji wa huduma bora kwa jamii kwa lengo la kuinua ubora na kiwango cha ufaulu kwa mwaka 2022 ndani ya Halmashauri hiyo.
Baadhi ya mikakati ya kuinua kiwango cha ufaulu Mtama;-
- Kufanya ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji kwa shule za msingi na sekondari
- Kusimamia kufikia malengo ya ufaulu ya 95% kwa darasa VII, 100% IV na kidato cha II,IV kwa daraja I-III la ufaulu na daraja I,II kwa kidato cha VI.
- Kukamilisha mada kwa wakati.
- Kuunda kamati ya KKK ya Wilaya
- Kufanya mashindano ya KKK
- Kutoa mafunzo ya KKK (Kata, Wilaya na Taasisi nyingine
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.