Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emanuel Mbilinyi Novemba 23, 2021 amekabidhi mifuko 11 ya saruji kwa uongozi wa Msikiti wa Kijiji cha Pangatena ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa kwenye mkutano wa kijiji a lipotembelea kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi wa kijiji hicho, ambapo changamoto moja wapo ilikuwa ni kusuasua kwa ujenzi wa msikiti na kumuomba Mkurugenzi kutoa mchango wa hali na mali ili kuchagiza ujenzi huo.
Akikabidhi mifuko hiyo ya saruji, Ndg. Mbilinyi alisema kuwa yeye ni kiongozi wa madhehebu yote ya Kikristo na Kiislamu na kwamba atawaongoza wananchi wake kulingana na sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akiwasisitiza viongozi hao kudumisha mahusiano mazuri katika jamii bila kujali tofauti zao za kiimani.
Kwa upande wake Shekhe Salumu Hamisi Namiundu kwa niaba ya waumini wa msitiki huo alimshukuru Mkurugenzi huyo huku akiahidi kuwa saruji hiyo itaenda kutumika kikamilifu kwa malengo yaliyopangwa .
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo pia alichangia mifuko 7 ya saruiji katika ujenzi wa ofisi ya Kijiji cha Hingawali iliyofikia hatua ya boma kupitia nguvu na michango ya wananchi.
Aidha, alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa jamii kuendelea kushiriki kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekeleza na Serikali ya awamu ya 6 pamoja na kuhimiza kudumisha amani ikiwa ni tunu ya Taifa na kuwaombea viongozi kwani wanapitia mitihani mingi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.