Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi Oktoba 16 2021 ameshiriki kwenye sherehe za mahafali ya 13 ya kidato cha nne yaliyofanyika katika shule ya sekondari Ruo.
Sherehe hizo ziliambatana na matukio mbalimbali ikiwemo uzinduzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 52 pamoja na chumba maalumu cha kupumzika wagonjwa wa kike. Aidha mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo alipewa heshima ya kuongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya chumba cha kompyuta ambapo kiasi cha Tzs 797,000/= kilikusanywa papo hapo huku Tzs 1,070,000/= ikiwa ni ahadi na kufanya jumla ya Tzs 1,867,000/=.
Mbilinyi alitoa wito kwa wahitimu wa kidato cha nne kuongeza bidii, kuwa na ushirikiano, kuwa makini katika mitihani yao inayotarajiwa kufanyika Novemba 2021 na kiwaomba walimu wa shule hiyo kuendelea kutoa elimu na mafunzo bora ili kufikia malengo ya wahitimu hao. Sambamba na hilo Ndg. Mbilinyi amewataka wazazi kuhakikisha wanalipa ada za shule kwa muda muafaka ili kuendeleza shughuli mbalimbali za taasisi hiyo.
Jumla ya wanafunzi 61 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kwa mwaka 2021 ambapo kati yao wavulana 43 na wasichana 18 pamoja na wanafunzi wa kujitegemea 9 wasichana 6 na wavulana 3 hivyo basi kufanya jumla ya wanafunzi 70.
Mkurugenzi akimlisha keki muhitimu
Mkurugenzi ( aliyeshika kipaza sauti) akiongoza harambee ya uchangiaji kwa ajili ya chumba cha kompyuta
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.