Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg Samwel W. Gunzar, ametekeleza kwa vitendo agizo la Mhe, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuwaagiza Wakurugenzi Watendaji na Watendaji wengine kutokwenda likizo kwa ajili ya kusimamia ujenzi wa vyumba vya madarasa na utengenezaji wa samani ili kuwawezesha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na masomo ya kidato Cha kwanza 2021 wasipate taabu. Mkurugenzi huyo amefanya ziara Tarehe 10 Disemba 2020 kwa kutembelea miradi mbalimbali ya ujenzi ikiwemo Shule ya Sekondari Mnara. Aidha amekemea vikali kwa Watendaji pamoja na wajumbe wa kamati za ujenzi kwa spidi ndogo, na kuwaagiza kusimamia ujenzi huo usiku na mchana.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.