Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama Ndugu George E. Mbilinyi amewataka watumishi wa ajira mpya za serikali waliopo Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kuwajibika kwa umma hili kuleta maendeleo na kuacha alama chanya ya utumishi wao kwa Halmashauri na Serikali kwa ujumla.Ndugu Mbilinyi alisema hayo katika kikao chake pamoja na watumishi wa ajira mpya idara ya Uvuvi, Kilimo na mifugo.
Ndugu Mbilinyi aliongeza kua maafisa hao wanapaswa kutumia elimu na weledi walionao kuleta mabadariko chanya katika Uvuvi, Kilimo na ufugaji kwa sababu wananchi wengi katika Halmashauri wanafanya shughuli hizo.
Aidha mkurugenzi mtendaji alimaliza kua watumishi wa ajira mpya wanapaswa kujiwekea marengo, kujiendeleza kielimu, kuheshimu tamadani pamoja na kufuata sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza utumishi wa umma, hivyo wataumishi wa ajira mpya wanapaswa kua na maadili na nidhamu kwa viongozi pamoja na wananchi.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.