Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mhe. George Mbilinyi ametoa fursa kwa wawekezaji kutoka ndani na nje ya Tanzania waweze kujitokeza kwa wingi ili kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali yaliyopo katika Halmashauri hiyo jambo litakalopelekea ongezeko la ukusanyaji wa mapato. Ameyasema hayo Septemba 08 2021 alipokuwa katika mahojiano na waandishi wa habari Mkoani Lindi na kuongeza kuwa ndani ya Halmashauri hiyo kuna maeneo mengi ya uwekezaji hivyo uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama umeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji watakaojitokeza.
Sambamba na hilo Mh. Mbilinyi amewaomba wageni wote wanaokwenda kwa ajili ya shughuli za kiofisi katika Halmashauri hiyo waweze kupata huduma ya malazi pamoja na chakula ndani ya Mji wa Mtama kwani kwa kufanya hivyo kutapelekea ongezeko la ukusanyaji wa mapato na kuweza kuwa chachu kwa wafanyabiashara mbalimbali kuboresha na kuendeleza biashara zao.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.