Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emanuel Mbilinyi amewataka wasimamizi pamoja na kamati za ujenzi wa miradi ya vyumba vya madarasa, vituo shikizi na vyoo kuwa na kasi kubwa katika usimamizi wa miradi hiyo ili kuendana na muda uliopangwa kukamilika kwake.
Rai hilo amelitoa leo Novemba 10, 221 alipokuwa kwenye ziara ya kikazi kukagua maendeleo ya miradi hiyo Tarafa ya Sudi na kuonekana kutoridhishwa na utendaji wa kazi huku akisema kuwa kulegalega kwa usimamizi kutapelekea Halmashauri hiyo kuwa nyuma kumaliza kwa ujenzi unaoendelea hivyo basi ni lazima nguvu ya ziada itumike ili kufikia lengo lililokusudiwa.
Amewataka wasimamizi pamoja na kamati za ujenzi :
• Kuwa site kila siku na kutoa taarifa kuhusu hatua ya ujenzi ilipofikia.
• Kutumia akili na maarifa katika utatuzi wa changamoto mbalimbali
• Kupeana majukumu ya kufanya na kusimamia
• Kufanya kazi na maamuzi kwa uwazi ili kila mmoja afahamu hatua mbalimbali zinazoendelea.
• Kuongeza nguvu kazi itakayosaidia kusukuma kwa kasi miradi hiyo.
• Hadi kufikia tarehe 20 mafundi wawe wamemaliza kumwaga zege ili hatua ya msingi ianze haraka.
Aidha amewataka walimu kutowaachia walimu wakuu peke yao na badala yake wanatakiwa kutoa ushirikiano mkubwa ikiwa ni sehemu ya majukumu yao na kwa kufanya hivyo watakuwa wameunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.