Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Mbilinyi Januari 31, 2022 katika kikao cha Baraza la Wafanyakazi kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano ambapo aliwataka wafanyakazi hao kwenda kutoa elimu pamoja na hamasa kwa jamii inayowazunguka ili waweze kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika mwaka juu 2022 nchi nzima. Aliongeza kuwa wanajamii wanatakiwa kuondoa fikra potofu juu ya zoezi hilo na badala yake waone umuhimu wa kuhesabiwa kwani kwa kufanya hivyo tutairahisishia Serikali kuandaa na kutoa huduma za kimaendeleo kulingana na mahitaji husika.
Aidha, Mbilinyi alitumia fursa hiyo kuwahimiza wajumbe wa Baraza hilo kila mmoja awajibike katika eneo lake la kiutendaji kwa kuongeza juhudi na maarifa hali itakayosaidia kuijenga na kuiendeleza Halmashauri hiyo. Sambamba na hilo, amewaomba wajumbe hao kushirikiana katika kuinua mapato kwa kuhakikisha watu wanalipa ushuru kulingana na shughuli wanazozifanya huku akiwahimiza wataalamu wa Idara ya Ardhi kuhakikisha wanapima maeneo mbalimbali yatakayouzwa kwa wananchi ili kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo.
Kwa hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesikitishwa na kasi ya kuripoti kwa wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kuwa ndogo licha ya kuwepo kwa miundombinu ya kusomea hususani madarasa yaliyojengwa hivi karibuni. Hivyo basi, ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto shule lengo ni kwenda sambamba na jitihada za Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.