Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwa kufanya jitihada kubwa ya kuzingatia suala la lishe kwa kufanya vikao vya mara kwa mara kulingana na mujibu wa Kalenda pamoja na jitihada wanayozozifanya katika kuwasilisha taarifa Mkoani.
Ndemanga ameyasema hayo tarehe 06/12/2021 aliposhiriki katika kikao cha Kamati ya Lishe na kuongeza kuwa zipo baadhi ya Halmashauri ambazo zinafanya vikao hivyo mara chache na wengine kutofanya kabisa, jambo linalosababisha changamoto katika ngazi ya mkoa kwa kutojua nguvu ziwekezwe vipi katika Halmashauri ili tatizo la lishe liweze kumalizika.
Aidha, Licha ya vikao kufanyika mara kwa mara, bado Halmashauri ya Mtama na Mkoa wa Lindi kwa ujumla unaonekana upo nyuma kwenye maendeleo ya Lishe. Na hii ni kwa sababu ya Nyanja zingine tofauti na vikao kusuasua. Ndemanga amemuagiza Mkurugenzi na watendaji wengine, kufuatilia vigezo vingine vya lishe kama zoezi la mtoto kuchangia shilingi elfu moja na kujihusisha na shughuli au miradi inayohusiana na suala la lishe ili baadae waweze kutambua ni lipi halijafanyika na kuweka mazingira ya kulifanya.
Suala la lishe limekuwa likiendana moja kwa moja na changamoto ya Utapiamlo. Lindi ni kati ya Mikoa iliyo na tatizo hilo jambo ambalo limekuwa likiwashangaza wengi kwakuwa vyakula bora vyote vinapatikana kwa gharama nafuu na baadhi vimekuwa vikipatikana bure. Hivyo Ndemanga ameitaka Halmashauri ya Mtama kutathmini ni wapi kuna changamoto hii kwa ukubwa ili waweze kutoa elimu zaidi kwa wananchi wake kwa sababu vyakula vipo, lakini changamoto ni jinsi gani wanavitumia vyakula hivyo kuondokana na tatizo la utapiamlo.
Aidha, ameipongeza Halmashauri katika suala la ujenzi wa madarasa ya COVID 19 na kukiri kuwa Halmashauri hiyo ililegalega hapo awali, lakini kutokana na jitihada za usimamizi zinazofanywa hadi kufikia tarehe 15 mwezi Disemba Mtama inaweza kushika nafasi ya kwanza katika Halmashauri zinazofanya vizuri kwenye ujenzi wa madarasa hayo. “Tunaweza tusimalize madarasa yote kwa asilimia mia moja, lakini na sisi tutakuwa na madarasa yaliyokamilika, lakini hatutokuwa na darasa lililo katika msingi…” Ndemanga.
Licha ya miradi hiyo kuhitaji jitihada kubwa ya usimamizi kwa sasa kutoka Halmashauri, bado amewataka viongozi kutoisahau miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa Wilayani humo.
Wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.