Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Ndemanga leo tarehe 14, Febuari 2024 ameongoza kikao cha kamati ya msingi ya afya ili kujadili maandalizi katika zoezi la utoaji chanjo ya SURUA RUBELLA, chanjo hiyo itatolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 yenye lengo la kujikinga na ugonjwa huo.
Mganga mkuu wa Halmashauri ya Mtama Daktari Dismas Masurubu alisema kuwa zoezi la utoaji wa chanjo litafanyika kwa muda wa siku nne mfululizo kuanzia kesho tarehe 15 hadi tarehe 18 Febuari 2024 na aliongeza kuwa zoezi hilo litaambatana na utoaji wa chanjo zilizopita kwa watoto hao.
Aidha Ndugu Albert Mpokwa Mratibu wa chanjo wa Halmashauri alisema kuwa zoezi hilo litawafikia walengwa 18148, chanjo hizo zitatolewa katika vituo vyote vya afya ndani ya Halmashauri pia Halmashauri imeongeza vituo vingine maalumu ili kufanikisha zoezi hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E Mbilinyi alimshukuru Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa jimbo la Mtama Mheshimiwa Nape Moses Nnauye kwa kutoa gari litakalofanya matangazo ili kufanikisha zoezi hilo.
Mwisho Ndugu Ndemanga aliipongeza Halmashauri kwa kufanya vizuri katika utoaji wa chanjo zilizopita hivyo anaamini kuwa Halmashauri itaendelea kufanya vizuri katika utoaji wa chanjo hizo lakini pia aliwataka wakuu wa idara, viongozi wa chama cha mapinduzi, waheshimiwa madiwani, Watendaji kata na vijiji na viongozi mbalimbali kuweka juhudi ili kufanikisha zoezi hilo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.