Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe: Victoria Mwanziva Ameyasema hayo Leo tarehe 30 Oktoba 2024 katika maadhimisho ya siku ya Lishe kiwilaya yaliyofanyika katika kata ya Namangale ndani ya Halmashauri ya Mtama.
DC Mwanziva aliongeza kuwa bustani hizo zitasaidia upatikanaji wa mbogamboga za majani pamoja na matunda Kwa Wanafunzi ndani ya mwaka mzima bila kujali msimu ambapo upatikanaji huo wa mbogamboga utasaidia utoaji wa lishe bora Kwa watoto waliopo mashuleni.
Aidha Bi: Emma Lunojo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mtama alisema kuwa katika kutekeleza afua za lishe Halmashauri ya Mtama Kila mwaka inatenga Shilingi elfu moja(1000) Kwa Kila mtoto aliye na umri chini ya miaka 5 lakini pia Halmashauri inaendelea kutoa elimu ya ulaji chakula bora kwa wajawazito, watoto wenye umri chini ya miaka 5 na makundi rika.
Kwa upande wa Afisa Lishe ngazi ya Mkoa Bi: Juliana Chikoti amewasisitiza wakazi wa Namangale kuzingatia ulaji wa mlo kamili Kwa kuzingatia makundi sita ya vyakula ili kuhakikisha jamii yetu inakuwa mbali na magonjwa sugu yasiyoambukiza.
Mwisho Ndugu Hudhwaifa Rashidi katibu Tawala Wilaya ya Lindi amewahimiza Wananchi kuhakikisha wanazingatia elimu iliyotolewa na Wataalamu lakini pia kushiriki zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika Novemba 27 mwaka huu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.