Moto huo umetokea siku ya tarehe 26 Septemba 2021 majira ya saa nne usiku kwenye shule ya sekondari Mahiwa iliyopo Kata ya Nyangao Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na kusababisha kuteketea kwa vitu vyote vilivyokuwepo katika daharia hilo vikiwemo vitanda, magodoro pamoja na madaftari ya wanafunzi. Waathirika wa janga hilo ni baadhi ya wanafunzi wavulana kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne waliokuwa wakiishi kwenye bweni hilo na kwamba katika tukio hilo hakuna mwanafunzi yeyote aliyepata majelaha ama kupoteza maisha.
Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama umewataka wanafunzi hao kutokuwa na hofu na badala yake waendelee na masomo kama kawaida kwani unaendelea na taratibu za kutoa msaada wa haraka ili kuhakikisha wanafunzi hao wanakuwa katika mazingira rafiki na salama. Aidha, kwa pamoja Mkuu wa Wilaya ya Lindi Ndg.Shaibu Ndemanga, Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. Mahmoud Kimbokota , Afisa Elimu Sekondari Wilaya Mwl. Mwinjuma Rajabu Mumini wamewaomba wadau mbalimbali wajitokeze kwa wingi kuweza kutoa michango yao ya hali na mali ili kuwapa faraja waathirika hao.
Taarifa za chanzo cha moto huo, tahmini pamoja na takwimu sahihi ya vitu vilivyoteketea zinatarajiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi Mtatiro Kitinkwi mara baada ya uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilika.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.