Kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kilichoketi tarehe 29 Januari 2021, kimepitisha bajeti ya awali ya Tshs. 26,511,168,253/= kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022. Vyanzo vya mapato hayo ni kutoka 1.Serikali kuu. 2. Halmashauri ya Wilaya. 3. Wahisani. Bajeti hiyo imeandaaliwa kwa kuzingatia Ilani ya CCM 2020-2025, Dira ya Taifa ya Maendeleo, Hotuba ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uzinduzi wa Bunge la 12 na pia Sera za kisekta. Bajeti hiyo itahusika katika matumizi ya Mishahara, Miradi ya Maendeleo pamoja Matumizi mengine. Hivyo bajeti ilipewa baraka zote na wajumbe . Baadhi ya wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti na Katibu wa CCM wa Wilaya, Katibu Tawala wa (W) na Wataalamu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.