Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mheshimiwa Yusufu Tipu Leo tarehe 28 Febuari 2024 ameongoza Mkutano wa Baraza la Madiwani, Baraza hilo limeridhia kupitisha rasimu ya bajeti ya Shilingi Bilioni 30,128,756,500.00 kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Aidha Waheshimiwa Madiwani wameonesha kuwa na Imani na maono chanya katika maandalizi ya mipango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 ikiwemo Baraza la wafanyakazi, kamati ya ukimwi, kamati ya elimu, kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira, kamati ya fedha, Utawala na mipango.
Hata hivyo katika Baraza hilo la kupitisha rasimu ya bajeti Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E Mbilinyi amewapongeza Waheshimiwa Madiwani wa kata zote kwa kuwa wafuatiliaji wa miradi ya maendeleo na michango yao katika kuendeleza Halmashauri, Pia ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha za kuendeleza miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji, barabara, umeme, ujenzi wa shule na vituo vya Afya.
Vilevile, katika Mkutano huo walikuwepo wawakilishi kutoka TARURA, RUWASA, na TANESCO ambapo Kila mmoja alielezea mipango ya kuongeza na kuboresha huduma wanazozitoaza kwa wananchi wa Mtama. TARURA walieleza kuwa bajeti yao ni shilingi Bilioni 3.6 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara ndani ya Halmashauri.
Pia Mwenyekiti wa Halmashauri aliishukuru Serikali na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia thabiti ya kuboresha maisha ya Watanzania, pia alimshukuru Mkurugenzi na wataalamu wa Halmashauri kwa ushirikiano wa kuleta maendeleo katika Halmashauri, Mwisho alisisitiza kwa Waheshimiwa Madiwani kuwa Serikali inafanya mambo mazuri na makubwa hivyo ni jukumu la madiwani kutangaza mambo hayo kupitia mikutano ya hadhara katika kata zao.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.