Mafunzo ya matumizi bora na sahihi ya Mfumo wa taarifa za Shule ya msingi kwa wakuu wa Shule za Msingi (SIS) katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi ni mwendelezo wa Mafunzo mbalimbali ya kuwajengea uwezo
wakuu hao yanayoandaliwa na program ya EQUIP T katika Mkoa wa Lindi. Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Shule ya Msingi Nyangao kuanzia Tarehe 21/01 hadi 24/01/2019, Jumla ya wakuu wa Shule 117 wa Shule zote za Msingi wamehudhuria katika kupata Dozi hiyo. Mafunzo hayo yamewezeshwa na Wawezeshaji 9 kutoka ngazi ya kitaifa wakiongozwa na Ndg Sophia K. Mnyanyi kutoka OR-TAMISEMI, Idara ya Elimu ambaye anashughulikia Takwimu mbalimbali za Shule zote za Msingi.
Msisitizo mkubwa umetolewa kwa wakuu wa Shule wote wa namna ya uingizaji wa takwimu sahihi na kwa wakati kwa kila inapohitajika kufanya hivyo, aidha kuhuisha takwimu hizo mara pale panapotokea mabadiliko yoyote.
Katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Eng. Mbaraka Kilangai, aliwaomba washiriki wote wa mafunzo kuwahi muda wa mafunzo, kuwa wasikivu na kuuliza pale ambapo hapajaeleweka ili kuwa na ujuzi wa kutosha mara wamalizapo mafunzo haya na kuleta mabadiliko chanya ya matumizi sahihi ya kishikwambi katika Halmashauri ya Wilaya ya lindi. nae Afisa Elimu Msingi Wilaya Ndg Danstan J. Ntauka aliendelea kutoa msisitizo kwa washiriki kuwa wavumilivu na kuvitunza vishikwambi vyote kwa kipindi chote cha mafunzo na hata kwenye vituo vyao vya kazi. Kwa mujibu wa taratibu za program kwa yeyote anayepoteza kishikwambi atawajibika kukilipa, hivyo ili kuepuka hilo ni vyema kuvitunza.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.