Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe: Seleman Jafo(Mb) amewasisitiza Wananchi wa kata ya Mandwanga kutoharibu miundombinu ya maji kama vile mabomba na koki, Ameyasema hayo tarehe 21 Septemba 2024 alipotembelea na kukagua mradi mkubwa wa maji uliopo kata ya Mandwanga (Mandwanga Corridor) wakati wa ziara yake katika Halmashauri ya Mtama.
Mradi huo unaenda kuondoa tatizo la ukosefu wa maji safi na salama katika Vijiji nane vilivyopo katika kata hiyo vyenye jumla ya watu zaidi ya elfu 20, aidha alisisitiza pia Ruwasa kuhakikisha Wananchi wanapata huduma hiyo ya maji Kwa bei nafuu ili Kila mwananchi apate maji kulingana na mahitaji yake.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.