Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo tarehe 29 Julai 2024 imekutanisha Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutekeleza zoezi la ukusanyaji wa maoni ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025-2050, Zoezi hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Aidha zoezi hilo limehudhuliwa na wajumbe mbalimbali na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali ikiwemo vijana, wanawake, wazee, wakulima, wafanya biashara, watu wenye uhitaji maalumu, nyama vya siasa pamoja na Wakuu wa idara mbalimbali.
Akiongea na wajumbe hao Ndugu Shaibu Ndemanga Mkuu wa Wilaya ya Lindi alisema kuwa kila Mwananchi anatakiwa kushiriki kikamilifu katika utoaji wa maoni na kuhakikisha anajaza Dodoso kwa umakini na kwa usahihi ili kupata Tanzania iliyo bora zaidi.
Mwisho DC Ndemanga aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa lakini pia kujikinga na ugonjwa hatari wa kipindupindu kwa kuchukua tahadhari na kuzingatia usafi wa Mazingira.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.