Maelekezo hayo yametolewa Machi 17, 2022 na Katibu Tawala wilaya ya Lindi Mh. Mbwana Rajabu Kambangwa kwenye kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ambapo aliwataka wakuu wa Idara kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuhakikisha inakamilika kwa wakati na ubora unaoendana na thamani ya fedha.
Katibu Tawala alitoa maelekezo kwa mweka hazina wa Halmashauri CPA Asha Msangi kuongeza juhudi katika ukusanyaji wa fedha kwa kushirikiana na Mkurugenzi ili kuinua mapato yatakayosaidia kuendesha shughuli mbalimbali.
Aidha alitoa msisitizo kwa maafisa utumishi kujenga mahusiano mazuri na watumishi wao, kuwatumia ipasavyo Maafisa Tarafa kwenye majukumu mengine kwani wao ni viunganishi vya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa. Lakini pia ametoa maelekezo kwa Afisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu inarejeshwa kwa wakati.
Kwa hatua nyingine Mh. Kambangwa alitoa maagizo kuhusiana na utunzaji bora wa dawa katika vituo vya kutolea huduma lakini pia kuwa na ushirikiano na wananchi kwa kuwajibika pamoja na kutoa hufuma bora katika jamii.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi wote Ndg. Alfonse Ngongi alimshukuru Katibu Tawala huo kwa kutenga muda na kuahidi kuwa maelekezo yake yatatekelezwa ipasavyo.
Katibu Tawala aliitisha kikao hicho kwa lengo la kujitambulisha, kuwafahamu watumishi pamoja na kutoa maelekezo hayo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.