Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E. Mbilinyi anatoa pole kwa familia na watanzania wote kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1985-1995, Mheshiwa Ally Hassan Mwinyi, ambaye amefariki dunia jana Alhamis tarehe 29 Febuari 2024.
Aidha kufuatia kifo hicho, Mheshiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan ametangaza kuwa nchi yetu itakua katika kipindi cha siku saba za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo Machi 1, 2024. Hayati Ally Hassan Mwinyi atazikwa tarehe 2 Machi 2024 huko Unguja, Kisiwani Zanzibar.Inna lillahi wa inna ilayhi raaji'un.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.