Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama Ndugu George E Mbilinyi leo tarehe 22 February amefanya ziara katika Kituo Cha Afya Pangaboi kwa lengo la kusuruhisha mgogoro wa uzabuni, mgogoro huo unachelewesha mradi wa ujenzi katika Kituo hicho katika ziara hiyo Mkurugenzi alifanya kikao na kamati ya ujenzi wa Kituo hicho.
Kituo Cha Afya Pangaboi kilipokea kiasi Cha fedha milioni 500 kutoka Serikali kuu kwa lengo la ujenzi wa majengo manne ambayo ni jengo la uzazi na jengo la upasuaji (mbili kwa moja), jengo la maabara, jengo la kufuria na nyumba ya wafanyakazi ( tatu kwa moja), hivyo ujenzi huo ulisimama kutokana na mgogoro wa uzabuni.
Aidha Mkurugenzi alisuluhisha mgogoro huo kwa kuitaka kamati ya ujenzi ya Kituo hicho kuanza upya mchakato wa kumpata mzabuni na Kila hatua watakayo fikia lazima Mkurugenzi ahusishwe, hivyo aliitaka kamati hiyo kutangaza nafasi ya uzabuni na kamati hiyo ihakikishe kuwa ujenzi unaanza wiki ijayo.
Pamoja na hayo katika ziara hiyo Mkurugenzi aliambatana na wakuu wa idara kama ifuatavyo: mganga mkuu wa Halmashauri, Afisa ugavi na ununuzi wa Halmashauri, Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri na wajumbe mbalimbali, mwisho alizitaka idara ya Afya, idara ya ujenzi na kamati ya ujenzi ya Kituo hicho kuhakikisha hadi kufikia Mei 30, 2024 ujenzi uwe umekamilika.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.