Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg George Mbilinyi amefanya ziara na kuangalia maendeleo ya utoaji huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama. Moja ya maeneo aliyotembelea ni ujenzi wa zahanati ya Mahiwa ambapo alitoa maagizo kwa Mtendaji wa Kata .na Kijiji Pamoja na kamati ya ujenzi wa Zahanati kuangalia ni jinsi gani Wanaweza kutumia rasilimali za Kijiji kwa ajili ya kutengeneza dhamani za zahanati hiyo, Ameongeza kuwa kiu yake ni kuona zahanati hiyo inaaza kutoa huduma kwa wananchi haraka iwezekanavyo. Aidha amesisitiza usafi wa mazinga ufanyike ikiwa ni Pamoja na kufyeka nyasi na kupanda mauwa kwenye zahanati hiyo ya mahiwa iliyoko Kata ya nyangao.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.